Breaking News

Spika Ndugai Atia Neno Juu Ya Mauaji Ya Watoto Njombe



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ameiagiza Serikali kutoa kauli kuhusu mauaji ya watoto yanayoendelea mkoani Njombe ambayo yamezua gumzo hivi karibuni.

"Kumezuka taharuki kubwa na shughuli za uchumi hazifanyiki, wakinamama wanatakiwa kuwapeleka watoto wao shuleni na kuwarudisha jioni," amesema Spika huku akiitaka serikali kutoa majibu kabla ya kuahirishwa kwa mkutano wa Bunge Ijumaa Februari 8, 2019.

Kauli ya Spika ameitoa bungeni jijini Dodoma leo baada ya Mbunge wa Lupembe (CCM), Joram Hongole aliyetaka Bunge kuahirisha shughuli zake za leo ili kujadili mauaji hayo.

Mbunge wa Lupembe, Joram Hongole alisema taharuki imezuka mkoani Njombe na shughuli za uchumi zimesimama baada ya mauaji ya watoto mkoani humo.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama amesema kuwa wao kama serikali ili waweze kutoa maelezo ya kina wameomba wapewe nafasi kuandaa taarifa ambayo serikali imechukua.

No comments