FRONTPAGE: KWANINI MWINYI ZAHERA AMESEMA ANAENDA CONGO LAKINI YUPO NA AS VITA?
Taarifa zinasema kuwa Mwinyi Zahera kocha wa Yanga aliaga anakwenda Congo lakini wadukuzi wa mambo wakamfumania akiwa na makocha wa AS Vita na wachezaji.
:
Leo tukampigia Mwinyi Zahera na kutujuza kulikoni.........!!
: "Mimi ni mkongo kila mtu anajua hilo, inamaana sina haki ya kuongea na wakongo wenzangu kwa sababu mimi ni kocha wa Yanga?"
:
RIPOTA: Labda wangependa kufahamu haswa ulikwenda kuwaona kwa sababu zipi ili kuondoa utata?
:
ZAHERA:"Hao wanaouliza uliza kwanza niwape taarifa labda hawajui, mimi ni kocha msaidizi timu ya taifa ya Congo. Je ina maana kwakuwa Simba inacheza na AS Vita nakatazwa kuonana na wachezaji wa AS Vita ambao tumewaita timu ya taifa? Mimi mambo ya Simba yananihusu nini?"
:
RIPOTA: Kwahiyo kocha unashauri nini kwa wanaosambaza taatifa hizo?
:
ZAHERA:"Wajiandae kimbinu kupata matokeo chanya wala sio kutafuta hoja ambazo hazitawakua na msaada wowote kwao"
:
RIPOTA: Ushauri wako wa mwisho?
:
ZAHERA:"Kufanya kazi Tanzania hakuninyimi uhuru wangu kwa sababu tu hisia za watu fulani" Mwinyi Zahera.
:
Tumeelewana lakini?
Pata habari motomoto na za uhakika kila siku kila zinapojiri katika nyanja mbalimbali ikiwemo Siasa, Michezo, Ajira, uchumi, Mapenzi, Udaku/Umbea n.k .Kwa kudownload APP hii Bofya HAPA Kudownload.
BOFYA HAPA
No comments