KAMATI YA BUNGE YAHITIMISHA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI ILIYO CHINI YA WIZARA YA ELIMU
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imekamilisha ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi mitatu mikubwa inayogharimiwa na Serikali kupitia bajeti ya Mwaka 2018/19 katika baadhi ya Vyuo vilivyo chini ya Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia na kuridhishwa na utekelezaji wa Miradi hiyo.
Kamati hiyo imetembelea Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu (DUCE) katika mradi wa upanuzi na ukarabati wa jengo la Utawala ambalo linagharimu shilingi Bilioni 3.2 ambapo kazi hiyo inaendelea na litakapo kamilika litaongeza nafasi kwa ajili ya ofisi za watumishi na vyumba vya mikutano.
Aidha kamati imetembelea mradi wa upanuzi wa vyumba vya mihadhara
katika Chuo Kikuu Ardhi kazi ambayo imekamilika kwa hatua ya kwanza na
itagharimu shilingi Bilioni 2.5 hadi kukamilika kwake.
Kamati imekamilisha ziara yake katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, ambapo Wajumbe watembelea Jengo la jipya la Mihadhara linalojengwa kwa mapato ya ndani ya Chuo hicho, ambalo linauwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 300 kwa wakati mmoja. Aidha kamati imepongeza wizara na uongozi wa Chuo kwa kazi nzuri na kubwa iliyofanyika katika kusimamia ujenzi huo. Jengo hilo limekamilika kwa asilimia 95.
Aidha Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Joyce Ndalichako amepongeza uongozi wa Chuo kwa kusimamia vema matumizi ya fedha za zinazotokana na Mapato ya ndani na kutumika kwa kutekeleza miradi yenye tija kwa Chuo. Ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh John Pombe Magufuli kwa kusimamia suala la kubana matumizi na kuelekeza fedha katika kazi zenye faida kwa jamii kama ilivyo kwa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Katika majumuisho ya ziara hiyo, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mh. Oscar Mukasa(Mb) ameipongeza wizara na taasisi zilizotembelewa kwa kusimamia utekelezaji wa miradi na kushauri taasisi hizo kujikita katika kusimamia Dira na dhima za uanzishwaji wake. Kamati pia imeshauri Serikali kupitia Wizara kuhahakisha inatoa fedha za miradi kwa wakati kulingana na bajeti.
Imetolewa na:
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini,
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
18/3/2019
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini,
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
18/3/2019
Pata habari motomoto na za uhakika kila siku kila zinapojiri katika nyanja mbalimbali ikiwemo Siasa, Michezo, Ajira, uchumi, Mapenzi, Udaku/Umbea n.k .Kwa kudownload APP hii Bofya HAPA Kudownload.
BOFYA HAPA
No comments