Mazoea yaziponza Yanga na Simba
Shirikisho la soka nchini (TFF), limeashusha rungu kali kwa vilabu vikongwe nchini vya Simba na Yanga baada ya timu hizo kukiuka kanuni za mpira wa miguu kwa kutenda makosa kadhaa kwenye ligi kuu.
Akiongea leo kwenye makao makuu ya TFF, Afisa habari wa shirikisho hilo, Cliford Ndimbo amesema kamati ya saa 72, imepitia makosa mbalimbali ya timu za ligi kuu ikiwemo Simba na Yanga hivyo kutoa adhabu kwa mujibu wa kanuni.
Mabingwa watetezi Simba na vinara wa ligi msimu huu Yanga wametozwa faini ya jumla ya shilingi milioni 9, kwa kutumia mlango usio rasmi kuingia uwanja wa taifa kwenye mchezo wa watani hao wa jadi Februari 16, 2019.
Yanga ambayo ilijikusanyia jumla ya milioni 165,215,792.86 kwenye mchezo huo imepigwa faini ya shilingi milioni 9 wakati Simba wakitozwa shilingi milioni 3.
KLABU ya Simba imetozwa faini ya milioni tatu kwa kuingia uwanjani wakitumia mlango usio rasmi, lakini vilevile kutotumia njia maalum iliyowekwa kwa ajili ya kuingia kwenye eneo la kuchezea . Adhabu imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mbali na hilo Yanga imepata pigo kwenye eneo lake la ulinzi baada ya Kamati ya Nidhamu ya TFF, kumtia hatiani mchezaji Abdallah Shaibu kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Coastal Union na kamati kumfungia mechi tatu mfululizo/zinazofuatana kwa mujibu wa kifungu cha 48(1)(d) cha Kanuni za Nidhamu TFF.
Kamati ya Nidhamu ya TFF, imemtia hatiani mchezaji wa Young Africans Abdallah Shaibu kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa timu ya Coastal Union,Kamati imempa adhabu ya kufungiwa mechi tatu mfululizo/zinazofuatana kwa mujibu wa kifungu cha 48(1)(d) cha Kanuni za Nidhamu TFF.
Pata habari moto na za uhakika kila siku kila zinapojiri katika nyanja mbalimbali ikiwemo Siasa, Michezo, Ajira, uchumi, Mapenzi, Udaku/Umbea n.k .Kwa kudownload APP hii Bofya HAPA Kudownload. BOFYA HAPA
No comments