Serikali yatoa mapendekezo ya bajeti 2019/2020
Amesema serikali inapanga kutumia jumla ya shilingi trilioni 33 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo huku kati ya fedha hizo shilingi trilioni 20.5 zikitengwa kwa matumizi ya kawaida ikijumuisha gharama za uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na maandalizi ya uchaguzi mkuu 2020.
Pia gharama za matumizi ya maendeleo zinatarajiwa kuwa shilingi trilioni 12.4 ambapo kati ya hizo, shilingi trillion 9.3 ni fedha za mapato ya ndani na trilioni 2.1 ni za nje.
Kwa upande wake Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya uwasilishaji huo amewataka mawaziri wote kuhakikisha wanahudhuria vikao vya kamati za bunge hasa pale wanapohitajika ili kuweza kutoa ushirikiano katika uboreshaji wa bajeti.
Baadhi ya wabunge pia wamezungumzia mapendekezo hayo baada ya Waziri Mpango kuwasilisha mpango huo, ambapo wameeleza jinsi bajeti hiyo ilivyo kuwa na changamoto ambazo zinahitaji kutatuliwa kabla ya kykamilishwa kwake.
Hata hivyo serikali imesema itaendeleza mapambano dhidi ya rushwa ili kuimarisha ulinzi wa rasilimali na kudhibiti matumizi ya fedha za umma.
Pata habari motomoto na za uhakika kila siku kila zinapojiri katika nyanja mbalimbali ikiwemo Siasa, Michezo, Ajira, uchumi, Mapenzi, Udaku/Umbea n.k .Kwa kudownload APP hii Bofya HAPA Kudownload. BOFYA HAPA
No comments