Taarifa kutoka NIDA kuhusu vitambulisho vya taifa kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam
#TAARIFA
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inawakumbusha wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza kuchukua Vitambulisho vya Taifa katika ofisi za Serikali za Mitaa walipojiandikisha.
Kuwa na kitambulisho cha Taifa kutakusaidia mwananchi kupata huduma mbalimbali kama; kusajili laini za simu, kupata leseni za biashara na udereva, kusajili kampuni, kupata TIN, kupata hati ya kumiliki ardhi, kupata hati ya kusafiria(paspoti), kujidhamini na kudhaminiwa, kukopesheka kirahisi na kufungua akaunti benki.
Wananchi ambao hawajasajiliwa wafike ofisi za usajili za NIDA katika wilaya wanazoishi ili wasajiliwe.
Pata habari motomoto na za uhakika kila siku kila zinapojiri katika nyanja mbalimbali ikiwemo Siasa, Michezo, Ajira, uchumi, Mapenzi, Udaku/Umbea n.k .Kwa kudownload APP hii Bofya HAPA Kudownload.
BOFYA HAPA
No comments