TRA YATOA MSAADA WA BIDHAA ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILL 14.3 KWA WATU WENYE MAHITAJI MAALUMU
Mamlaka ya Mapato Nchini TRA MkoanI Mara imetoa msaada wa bidhaa mbalimbali kwenye taasisi za serikali na zisizokuwa za serikali ili kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu wakiwemo watoto na wazee.
Akikabidhi bidhaa hizo Meneja TRA Mkoa wa Mara Wallace Mnkande alisema kuwa wameamua kugawa bidhaa hizo ambazo baadhi yao zilikamatwa sababuya wafanyabiashara kukiuka tararibu za Kiforodha na muda wake wa kukaa pale kuisha nakuamua kuzigawa kwa taasisi zenye mahitaji.
“Bidhaa hizi baadhi yao zilikuwa zikielekwa nje ya Nchi na nyingine kuingia ndani ya Nchi yetu na baadhi kufuata taratibu zote lakini wanapopatiwa jumla ya tozo wanashindwa kulipia na kupewa muda lakini sasa muda wake umeisha na kuamua kutaifisha nakuzigawa ili jamii inufaike” alisema Meneja TRA Mara.
Mnkande aliwataka wafanyabaishara wote kufuata taratibu na kutimia njia rasmi katika kuingiza na kutoa bidhaa mbalimbali nje ya Nchi huku wananchi wakidai sitakabadhi pale wanaponunua bidhaa.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa TRA Mkoa wa Mara Wallace Mnkande kipindi akikabidhi Msaada wa bidhaa mbalimbali kwa Tasisi zikiwemo za serikali ili kuwasaidia watu wenye mahitaji wakiwemo watoto yatima, Wazee pamoja watu wasiojiweza.
Pia Wallace aliwataja bidhaa hizo zilizogawiwa katika taasisi hizo kuwa zinajumla ya shilingi Millioni 14.3.
Aidha wanufaika wa bidhaa hizo wametoa shukrani kwa mamlaka ya mapato Nchini TRA Mkoa wa Mara kwa kuwapatia bidhaa hizo kwa ajili ya Vituo vye Mahitaji wakiwemo Wazee na Watoto yatima.
Meneja TRA Mkoa wa Mara Wallace Mnkande aliyevaa miwani kutoka kushoto na koti jeusi akikabihi bidhaa hizo kwa taasisi mbalimbaloi zilizokuja kupokea msaada huo.
No comments