Breaking News

Urusi yapiga marufuku ndege za Boeing 737


Urusi ni kati ya nchi zilizopiga marufuku ndege aina ya Boeing 737 Max baada ya ajali ya Ethiopian Airlines.

Urusi imeongezwa katika nchi ambazo zimezuia ndege aina ya Boeing 737 Max baada ya ajali ya ndege ambayo ilisababisha vifo cha watu 157 nchini Ethiopia.

Ndege za Boeing 737  hazitaruhusiwa kuingia katika anga za Urusi.

Shirika la ndege la Rosaviatsiya limesema kuwa Ndege ya Boeing 737 imepigwa marufuku atika anga ya Urusi.

Hapo awali, ndege ya Urusi ilitangaza kwamba haitoruhusu kuruka kwa ndege hizo angani.

Maamuzi haya yalifanywa katika miezi sita iliyopita kutokana na kuanguka kwa ndege mbili za Boeing 737 Max.

Siku ya Jumapili ndege iliyokuwa ikitokea katika mji mkuu wa Ethiopia wa Addis Ababa,ilianguka na kusababisha vifo vya watu  157 muda mfupi baada ya kupaa.

 Nchini Indonesia ndege aina hiyohiyo ilianguka na kusababisha vifo vya watu 189 mwezi Oktoba mwaka jana.

Nchi nyiingi zimepiga marufuku ndege hizo baada ya ajali nchini ındonesia.



Pata habari motomoto na za uhakika kila siku kila zinapojiri katika nyanja mbalimbali ikiwemo Siasa, Michezo, Ajira, uchumi, Mapenzi, Udaku/Umbea n.k .Kwa kudownload APP hii Bofya HAPA Kudownload.
BOFYA HAPA

No comments