7 wapoteza maisha kutokana na mafua ya nguruwe
Watu saba wamepoteza maisha kutokana na mafua ya nguruwe Mongolia.
Kulingana na shirika la Shinhua, Waziri wa Afya wa Mongolia Davaajanstan Sarangerel, amesema kuwa watu saba wamepoteza maisha kutokana na mafua ya nguruwe toka mwanzoni mwa mwezi Januari.
Homa hiyo husababishwa na virusi vya H1N1.
Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), virusi vya H1N1 huenea kwa urahisi miongoni mwa watu, sawa na virusi vya mafua ya msimu.
No comments