Breaking News

Bodi ya wadhamii ya TFF yatoa onto Kali.


Baraza la wadhamini la Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limeonya kuwa kitendo cha baadhi ya wadau kupeleka masuala ya soka katika mahakama za kiraia kutasababisha Tanzania kufutiwa uenyeji wa fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 ambazo zimepangwa kufanyika hapa nchini mwezi Aprili mwaka huu.

Aidha balaza hilo limetoa rai kwa shirikisho kuhakikisha linaedeleza jitihada mbalimbali za kuwaondoa wabadhilifu was Mali za shirikisho.

Bodi ya Wadhamini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) leo Ijumaa tumeamua kuzungumza nanyi kuhusiana na hali ya Shirikisho.

Muda mwingi tumekua kimya ukimya ambao ulikua ukiendelea kutazama mambo mbalimbali yanavyokwenda ndani ya Shirikisho.


Bodi ya Wadhamini tunaunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na uongozi wa TFF chini ya Rais wake Wallace Karia tokea wameingia madarakani.

Kwetu tunajivunia mafanikio ambayo yamepatikana na yameonekana ndani ya kipindi kifupi cha mwaka mmoja.

Tumeona timu zetu za Taifa zimefanya vizuri katika mashindano mbalimbali na tumeshuhudia timu ya Taifa ya Vijana U17 ikichukua Ubingwa wa Cecafa U17 pale nchini Burundi lakini pia ikifanikiwa kuchukua Ubingwa kwenye mashindano ya ukanda wa COSAFA U17 na ikimaliza nafasi ya 3 kwenye mashindano ya kufuzu Afcon ya Vijana U17 Kanda ya CECAFA.

Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania Bara Kilimanjaro Queens nayo ilifanikiwa kuchukua ubingwa wa CECAFA kwa Wanawake nchini Rwanda na ikabeba ubingwa wa Jumuiya ya Afrka Mashariki nchini Burundi.

Timu ya Taifa ya Beach Soccer imefanikiwa kucheza fainali za Afrika za mchezo huo kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu,Vilevile Taifa Stars bado inapigania nafasi ya kufuzu Afcon 2019.

Hakika yote haya ni mafanikio makubwa katika mpira wetu na inaonesha mwenendo mzuri wa TFF na ndio maana sisi Bodi ya Wadhamini tunaunga mkono juhudi hizo.

Tunawaasa wadau wa mpira wa miguu kufuata na kuziheshimu taratibu zilizowekwa na zinazoendesha mpira wa miguu.

Tunafahamu Tarehe 2 Februari kuna Mkutano Mkuu wa mwaka wa TFF utakaofanyika Arusha tunawaomba wajumbe wa Mkutano Mkuu kuunga mkono jitihada hizi zinazofanywa na Uongozi wa TFF.

Tunawatakia Mkutano Mkuu mwema na tunaamini Wajumbe watajikita katika masuala mbalimbali yatakayosaidia katika maendeleo ya mpira wa miguu.

Hatua zote za kuwafungia wabadhirifu wa rasilimali za TFF na mpira wa miguu kwa ujumla wake tunaziunga mkono na tunaipongeza TFF wasiishie hapo waendelee kuwachukulia hatua wote wanajihusisha kwenye masuala hayo ya ubadhirifu.

Bodi ya Wadhamini tutaendelea kuunga mkono jitihada zote za TFF kuelekea kwenye maendeleo chanya.

Ahsanteni

No comments