Ebitoke “Itabaki Kuwa Siri YANGU Kwanini Nilitoka TIMAMU..Mkijua Hakika Mtanionea Huruma”
Mchekeshaji Ebitoke amejikuta kwenye wakati mgumu mara baada ya kupokea lawama nyingi kutoka kwa mashabiki wake kufuatia hatua yake ya kujiondoa kwenye kundi la Timamu.
Licha ya kuandamwa huko, Ebitoke amewaeleza kamwe hatoweza kuwaambia sababu iliyopelekea kujitoa kwenye kundi la Timamu.
Ebitoke alijizolea umaarufu mkubwa ndani ya kundi la Timamu akiwa na wachekeshaji wengine kama Mkaliwenu, Bwana Mjeshi, Mamaa Ashura, kwa sasa Ebitoke ameondoka kwenye kundi hilo.

No comments