Hatimaye Uwoya Naye amuanika Mpenzi Wake Mpya

Msanii wa filamu bongo anayetikisa kwa kula bata zaidi, Irene Uwoya, ameweka wazi juu ya mahusiano yake mapya aliyonayo, baada ya kuachana na aliyekuwa mumewe Dogo Janja.
Akizungumza kwenye sherehe za uzinduzi wa foundation ya msemaji wa Simba Haji Manara, Irene Uwoya amesema kwamba ni kweli kwa sasa yupo kwenye mahusiano, na mpenzi wake huyo ni mfanyabiashara.
“Ofcourse nipo kwenye mahusiano, yeye ni mfanyabiashara ila siwezi kuwatajia jina”, amesema Irene Uwoya.
Irene Uwoya kwa muda mrefu amekuwa akihisiwa kuwa kwenye mahusiano na mmoja wa wafanyabiashara wakubwa bongo, na kuaminiwa kuwa ndiye anayewezesha bata zote za msanii huyo, ingawa mwenyewe alikuwa anaficha ukweli wa jambo hilo.
No comments