Hatimaye Yanga Wapoteza Mchezo Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu Tanzania bara, Yanga sc hatimaye leo wamepoteza mchezo wa kwanza wa ligi baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya wapiga debe wa Shinyanga, Stand United katika mchezo uliopigwa dimba la CCM Kambarage.
Bao pekee la mchezo huo limewekwa kimiani na Jacob Masawe mnamo dakika ya 88 ya mchezo kunako kipindi cha pili.
Licha ya Yanga kupoteza mchezo huo bado wanaendelea kusalia kileleni mwa ligi hiyo huku wakiwa na pointi 53.

No comments