Je wajua? Chimbuko la kahawa ni nchi gani...
Je, unajua kwamba kahawa ilipelekwa mara ya kwanza mjini Istanbul kutoka Yemen katika karne ya 16 na kisha kahawa ya kituruki ikajulikana baada ya waturuki kuanza kuipika kwa namna yao.
Kulingana na baadhi ya hadithi "kahawa",ilipelekwa nchini Uturuki na wasyria wawili waliokuwa wanajulikana kwa jina la Hutm na Shems mwaka wa 1555.
Wakati wa utawala wa Sultan Süleyman ,kiongozi wa Yemen Özdemir Pasha, alifurahia sana baada ya kunywa kahawa hiyo na kaumua kuipeleka Ottoman na kumpa Sultan.
Baadaye, shirika la kahawa liliitengenezwa ndani ya hekalu ya mfalme na kuajiri watu wataalamu wa kupika kahawa.
Kahawa ya waturuki ilisambazwa ulimwenguni kwa mara ya kwanza mwaka 1615 na raia kutoka Vatican na baadae wafanyabiashara wa Marsilian walianza kuieneza Ulaya mwaka 1650.

No comments