Breaking News

Kamati Ya Bunge Yamhoji CAG , Wakati Kesi Ya Zito Na Spika Ikiruhusiwa..

Kamati ya Bunge ya Kinga, Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imemuhoji CAG, Professa Mussa Assad na imeahidi kufikisha taarifa yake kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wake, Emmanuel Mwakasaka, CAG ametoa ushirikiano ikiwemo kujibu maswali yote aliyoulizwa.

Hata hivyo katika hatua nyingine baada ya mahakama kuzuia kwa wiki nzima Ufunguaji wa Shauri la kikatiba, la kesi ya Zito Kabwe dhidi ya Spika,Job Ndugai  hatimaye shauri limefunguliwa.


Shauri hilo (Misc Civil Cause No. 1/2019 ) Zitto Zuberi Kabwe vs Job Ndugai ( Spika wa Bunge ) na linawakilishwa na Wakili Fatma Karume.

Kwa mujibu ya  post ya Zito Kabwe kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, amemshukuru wakili Karume  kwa juhudi alizoonyesha.

Aidha ameongeza kwa kusema kwamba licha ya kwamba tayari CAG amehojiwa na Kamati, Bado kuna haja ya kupata tafsiri ya kikatiba kuhusu Kinga ya CAG na kuhusu mamlaka ya Spika kushtaki Bungeni Wananchi wasio wabunge wanapotoa maoni yao. Tutaendelea na shauri hili kwa maslahi ya ulinzi wa Katiba ya nchi

No comments