Kufanyakazi nchini kinyume cha sheria kwamfikisha mahakamani
Mfanyabiashara Maarufu Nchini Kenya anayejihusisha na biashara ya madini katika mikoa ya Arusha na Manyara ambaye pia ni Wakili wa Kujitegemea, Raymond Nyange Ngoo mwenye miaka 37 mkazi wa Moshono Jijini Arusha amefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashitaka matatu.
Shitaka la kwanza linalomkabili mshtakiwa huyo ni pamoja na kuidanganya Serikali kuwa hajawahi kumiliki nyaraka za Serikali wakati alipopekuliwa alikutwa TIN namba na leseni ya udereva kinyume cha Sheria kwani yeye ni Mkenya na hakupaswa kuwa na nyaraka hizo kisheria.
Akisomewa Mashitaka na Waendesha Mashitaka wa Serikali Idara ya Uhamiaji, John Mwakasala, Adriano Mtambala na John Mkanyali mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha/Arumeru, Bernad Nganga mtuhumiwa alisomewa shitaka la pili la kufanya kazi katika Ofisi ya Uwakili ya Hakika Law iliyopo Arusha kama mtia saini tangu mwaka 2016 wakati akijua wazi kufanya hivyo ni kosa ikizingatiwa kuwa yeye siyo raia wa Tanzania.
Mwakasala amesoma shtaka la tatu ni kufanya biashara nchini bila ya kuwa na vibali halali wakati akijua wazi kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria, mtuhumiwa alikana mashitaka yote na yuko nje kwa dhamana ya watu wawili
No comments