Breaking News

Masau Bwire Kuunguruma Kesho TBC Taifa

Jumamosi, January 19, 2019, kuanzia saa 12.00 asubuhi, Afisa Habari wa Ruvu Shooting,  Masau Kuliga Bwire, na  Afisa Michezo wa Kikosi cha Jeshi, 832, Ruvu JKT, Cap Stanley Chahe, watakuwa mubashara television ya Taifa (TBC 1) kuzungumzia juhudi za pamoja za ujenzi wa uwanja wa Mabatini, kuondoa bati na kuzungusha ukuta wa tofali.

Kwa taarifa na mchango zaidi jiunge nao kuitazama TBC 1, siku na wakati wa kipindi hicho kitakaporushwa.

Wote tunataka waje nyumbani, tuwapapase tukiwa nyumbani, tumeona si vema tunayopaswa nyumbani, tuyapeleke ugenini halafu tuseme tuko nyumbani, ndio sababu mara nyingi tunapokuwa nyumbani ya ugenini, tunaonekana kupungua na kuonekana wageni kwa wageni wetu.

Karibuni sana, tuungane pamoja,  tuitazame TBC 1, kuanzia saa 12.00 asubuhi.

Ahsante.

Masau Kuliga Bwire, Afisa Habari wa Ruvu Shooting (Mzalendo ).

No comments