Breaking News

Ofisa TAMISEMI Akerwa Na Wasiokuwa Na vyoo


Mratibu Kampeni ya #NyumbaNiChoo kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bwana Selemani Yondu ameeleza kusikitishwa na wananchi wasio na vyoo katika kata ya Nyimbili, halmashauri ya wilaya ya Mbozi, Songwe. Akiongea kwa mshangao, amewauliza wananchi inakuwaje mtu ana nguvu na mtanashati kwa nje ila nyumbani hana choo?
Akijibu hoja ya Bwana Selemani, diwani wa kata hiyo amesema wanaendelea na ufuatiliaji nyumba kwa nyumba na akaihakikishia timu ya uhamasishaji kwamba ofisi yake itasimamia kila kaya iwe na choo bora ndani ya wiki mbili.
#NyumbaNiChoo

No comments