Breaking News

UN WOMEN YAITAKA TANZANIA KUTOA TAARIFA YA MASUALA YA JINSIA:

Image may contain: 3 people, people smiling, people sitting, table, drink and indoor

 Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake (UN Women) limeitaka Tanzania kuhakikisha inaingiza masuala ya jinsia katika taarifa yake itakayotoa katika Mkutano wa kimataifa wa Jukwaa la Juu la Kisiasa (High Level Political Forum) utakaofanyika Mwezi Julai ,9-18 Jijini New York Marekani mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa UN Women Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika Dkt. Izeduwa Derex-Briggs alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa na lengo la kumpa taarifa ya mkutano wa 63 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake duniani utakaofanyika Mjini New York Mwezi Machi Mwaka huu.
Aidha Waziri Ummy pamoja na Kiongozi huyo walifanya mazungumzo na kubadilishana mawazo kuhusu maeneo ambayo shirika la UN Women linayafanyia kazi kwa kushirikiana na serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

No comments