+VIDEO: Kikosi Cha Simba Kilivyowasili Nchini Kikitokea Congo, Kocha Anena Haya.
WAWAKILISHI pekee wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa, Simba Sc wamewasili nchini usiku wa kuamkia Jumatatu 21.01.2019 wakitokea Kinshansa ambako walikua na mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi AS Vita.
VIDEO: SIMBA WALIVYOWASILI JIJINI DAR ES SALAAM.
Katika mchezo huo,Simba walikutana na dhoruha ya kipigo cha mabao 5-0 na kujikuta wakiporomoka hadi nafasi ya tatu kwenye kundi lake linaloongozwa na Al Ahly ya Misri yenye pointi nne.
Mchezo huo ulikuwa mgumu huku Simba wakionekana kuwa na wakati mgumu licha ya kuanzisha muziki wake wote.
Tathmini ya kiufundi kwenye mchezo huo ilionyesha kwamba Simba ilizidiwa idara zote na Vita walitumia uzoefu wao kumaliza mchezo huo mapema.
VIDEO KOCHA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI.
No comments