Vyakula Vinavyoongeza Uwezo Wa Kujamiana: Part Ii
Chaza/Kilombwe (Oysters) ni mdudu wa baharini jamii ya kombe ambaye makazi yake ni kwenye miamba. Chaza huwa na Zinc, madini yanayosaidia mwili tukokeza testosterone homoni inayohusika kuendesha nyege kwa mwanamke na mwanaume.
Pilipili za Chile haitoi tu ladha nzuri mdomoni bali pia ina capsaicin kemikali inayochochea kutolea kwa endorphins kwenye ubongo inayomfanya mtu kujisikia vizuri. Mtu akiwa na furaha anaweza kufanya tendo la ndoa vizuri.
Asparaga (Asparagus) ni ana fulani ya maboga yenye vitamin B6, B9 & asidi ya foliki ambavyo huchochea msisimko na kufika kileleni(mshindo). Pia asparaga husaidia Vitamini E kuchochea homoni za ngono kwa wanaume na wanawake.
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili umethibitisha nyama ya pweza (supu ya pweza) inasaidia kuongeza hamu na nguvu ya kufanya tendo la ndoa.




No comments