Breaking News

FIFA wakubali kuendelea kuwapatia TFF Mamilioni ya fedha




Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema shirikisho la Mpira duniani FIFA limekubali kutoa gawaio la fedha ambazo zilizuiwa.

utakumbuka FIFA zilizuia kutoa fedha hizo kwa kipindi cha miaka mitatu kwa kile kinachodaiwa ni ubadhirifu wa fedha na matumizi mabaya kwa viongozi waliopita.

Karia ameeleza hayo leo Jijini Arusha upofanyika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Shirikisho hilo ambapo amesisitiza kuwa Katika uongozi wake hatasita kuwafungia wale ambao wanataka kutumia vibaya mali za taasisi hiyo.

Hatua hiyo ya FIFA kukubali kutoa fedha hizo imekuja baada ya uongozi wake (Karia) kusimamia vizuri matumizi ya taaisisi hiyo tangu uongozi wake ulipoingia madarakani.

No comments