KIKOSI MAALUM CHA KUPAMBANA NA UHALIFU NCHINI KIMEFANIKIWA KUWAKAMATA WAHUSIKA 30 WA MATUKIO YA MAUAJI MKOANI NJOMBE

Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas,ameongoza kikosi maalum katika kupambana na uhalifu nchini kilichoungana na vikosi vya jeshi la Polisi mkoa wa Njombe katika kufanya Operesheni katika mapori ya Nundu na Tanwat mkoani Njombe kuwasaka watuhumiwa wa Mauaji ya watoto. Picha na jeshi la Polisi

Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Nchini Naibu Kamishna DCP Liberatus Sabas, pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa Njombe Kamishina Msaidizi Mwandamizi SACP Afande Renata Mzinga wameongoza kikosi maalum cha kupambana na uhalifu nchini kilichoungana na vikosi vya Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe katika kufanya Operesheni katika mapori ya Nundu na Tanwat mkoani Njombe.(Picha na jeshi la Polisi)

Jeshi la Polisi Makao Makuu Kitengo Maalum cha Kupambana na uhalifu kikiongozwa na Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Naibu Kamishna Liberatus Sabas, kimeshirikina na Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe kuendesha Operesheni Maalum ya kukabiliana na matukio ya mauaji ya watoto wadogo ambayo yamejitokeza mkoani humo, mpaka sasa watuhumiwa 30 wamekamatwa waliojihusisha na matukio hayo,
Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Naibu Kamishna Liberatus Sabas, amesema watuhumiwa hao ifikapo Jumatatu watakuwa wamefikishwa Mahakamani kukabiliana na tuhuma za mauaji ya watoto, Aidha Naibu Kamishna Sabas, amewataka watanzania kutoa Taarifa za wahalifu popote walipo na amewahakikishia watanzania kuwa matukio hayo yamekoma sasa
Aidha Naibu kamishna Sabas amesema Jeshi La Polisi halitamuonea mtu yoyote haya awe Mfanyabishara, Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Dini, au Waganga wa Kienyeji watakaojihusisha na matukio ya mauaji kwa njia yoyote ile sheria itachukua mkondo wake huku akiapa kupambana na wahalifu wa mauaji yoyote yale kindakindaki
No comments