Madhara Yatokanayo Na Unywaji Wa Soda
Unapokunywa soda inakadiriwa vijiko 10 vya sukari vinakuwa vimeingia mwilini mwako dakika 10 tu baada ya kunywa soda. Hii ni sawa na 100% ya mahitaji yako ya siku. Hivyo unywaji soda mara kwa mara huelemea kongosho na kuongeza hatari ya kupata Kisukari.
Dakika 20 baada ya kunywa soda, kiwango cha sukari kwenye damu kinapanda na kufanya insulini kutolewa. Insulini ni kemikali itolewayo na kongosho ambayo hudhibiti umetaboli wa kabohaidreti (wanga) mwilini, upungufu wa insulini husababisha ugonjwa wa Kisukari.
Dakika 40 baada ya kunywa soda, mboni za macho hutanuka, shinikizo la damu huongezeka na ini lako huitikia kwa kuongeza kiwango cha sukari kwenye mfumo wa mzunguko wa damu unaohusisha moyo na mishipa ya damu.
Baada ya kunywa soda, kibofu hujaa na mtu kuhisi kukojoa hivyo kwenda kukojoa mara kwa mara. Kalisi (calcium), magnesi (magnesium) na zinki (zinc) zilizokuwa zitumike kwa ajili ya kuimarisha mifupa hupotea kwa njia ya mkojo. Pia maji, sodiamu na madini mengine hupotea.
Masaa zaidi ya mawili baada ya kunywa soda hali ya kujisikia furaha/vizuri (euphoria) huisha na sukari hupungua kwenye damu na kukufanya mwenye njaa, mchovu na mwepesi wa hasira.
Kwa kunywa soda unafanya mwili kupoteza virutubisho ambavyo vingetumika mwilini mfano kuimarisha mifupa na meno. Pia unywaji soda huongeza hatari ya kupata Kisukari.
Ndani ya dakika 20 baada kunywa soda, ini linaitikia kwa haraka na kubadili sukari yote na kufanya mafuta hivyo kumfanya mywaji soda wa mara kwa mara kuwa mnene.

No comments