Breaking News

Rais wa TFF afunguka kuhusu udhamini wa Ligi Kuu



Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema bado wanaendelea kutafuta mdhamini wa Ligi Kuu Soka Tanzania (TPL).
Karia ameeleza hayo leo Jijini Arusha upofanyika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Shirikisho hilo.
"Kuhusu udhamini wa ligi kuu tumeingia makubaliao na kampuni ya EAG kututafutia wadhamini, watu wanashindwa kuelewa kwamba si kwamba Vodacom wameondoka kuidhamini ligi yetu bali tumeshimdwa kufikia makubaliano ambayo naamini kama tungeyakubali kila mmoja wenu angetuona hatuna akili," ameeleza.
Ameendelea kwa kusema kuwa, 'Ili uthaminiwe nilazima ujithamini kwanza wewe, na sisi tumemua kujithamini wenyewe, hatutaki kuwa na mdhamini tu eti kwasbaabu ni fulani,'.

No comments