Breaking News

Takukuru yatakiwa kuchunguza viporo vya Simba



Wabunge ambao ni mashabiki wa Yanga wameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kulichunguza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa madai ratiba ya mechi za ligi kuu imekuwa ikiipendelea timu ya Simba.


Akizungumza jana Jumanne Februari 5, 2019, Mbunge wa Manonga (CCM), Seif Gulamali alisema anashangazwa na TFF kuibana kwenye ratiba timu ya Yanga huku ikiiacha timu ya Simba ikiwa haijacheza michezo mingi.


“Kwa mfano Yanga juzi imetoka kucheza na timu ya Coastal Union Tanga, halafu leo imepangwa kucheza na Singida United, halafu tena inarudi Tanga kucheza JKT, kwa nini wasingeacha mechi zinazochezwa Tanga ziishe ndiyo wapange kuwaleta Singida hasa ikizingatiwa ligi yenyewe haina mdhamini,” amesema.


Naye Mbunge wa Mpendae (CUF), Salim Hassan Turki amesema ameamua kutoa msaada wa mipira kwa kuwa yeye ni mwanachama hai wa Yanga na timu yake inapita kwenye kipindi kigumu hivyo ni vyema kushirikiana.


“Kuhusu hili figisu inaonekana lina ukweli, kwa kutumia vyombo hivi Takukuru waitazame TFF, pia isije kuwa inafanya mambo tayari asubuhi na mapema waanze kuchunguza hii viporo 11 vinakubalika kimpira?” Alihoji.

No comments