Breaking News



Timu ya Taifa ya Vijana U17 ya Tanzania (Serengeti Boys) imepangwa Kundi namba 1 kwenye Mashindano ya kimataifa ya Uefa Assist yatakayofanyika nchini Uturuki mwezi Machi.

Katika Kundi namba 1 Serengeti Boys imepangwa pamoja na Guinea,Australia ma wenyeji Uturuki.

Kundi namba 2 lina timu za Morocco,Cameroon,Uganda na Belarus wakati Kundi namba 3 lina timu za Senegal,Nigeria,Angola na Montenegro.

Mashindano yataanza Machi 1,2019 mpaka Machi 9,2019.

Serengeti Boys ambayo ipo kambini itatumia mashindano hayo kama sehemu ya maandalizi ya Fainali za Afrika U17 zitakazofanyika hapa nchini mwezi April.

No comments