TUSUBIRI HURUMA YA WAGANDA, IKISHINDIKANA TUSOME KITABU CHAO.
Muandishi maarufu wa Riwaya kutoka Nchini Marekani Brian Patrick Herbert kupitia Riwaya yake ya "The Sidney's Commet" aliandika maneno haya.
"The capacity to learn is a gift, the ability to learn is skills, the willingness to learn is Choice". Ntakupa tafsiri yake. Nisubiri.
Katika nyanja ya Mpira wa Miguu Nchini Tanzania Kuna changamoto nyingi kubwa ambazo tukianza kuhesabu Huwenda Akatukuta Masia. Suala la msingi ni kwamba Taifa jirani la Uganda limetokea kwenye changamoto kama za kwetu, waamuzi kuwa chini ya kiwango, miundo mbinu sio rafiki, mishahara midogo na kutopatikana kwa wakati kwa wachezaji na mengine kadhalika.
Kwa sasa taifa hilo limepiga hatua kubwa katika soka, Kama umesahau Uganda wanashiriki Afcon mara ya pili mfululizo ukiacha mara kadhaa walizoshiriki huko nyuma, huku sisi Tukiendelea kuwakumbuka Peter Tino, Juma Pondamali, ledger Tenga na mashujaa wengine wengi chini ya hayati Nkya Joel Bendera 'Mungu amrehemu'.
Uganda kwa miaka mingi wamekua wakifanya vema katika Ardhi ya Afrika mashariki hususan Cecafa challenji. Lakini mbawa zao kimataifa hazikua na nyuvu sana hivyo mwaka 2008 waliamua kukaa chini na kuandaa mpango mkakati wa kujitazama wanakosea wapi. Ashakum si matusi Uganda waliibuka na wazo la uwekezaji kwa vijana na kuanzia hapo kamati maalumu ziliundwa kwaajili ya kusimamia soka la vijana katika Kanda zote za uganda Sambamba na kuanzisha vituo vingi na kuviongezea nguvu vituo vya watu Binafsi.
Uganda kwa sasa wana vituo zaidi ya 90 vya serikali na binafsi vya vijana chini ya miaka 10- 15-17 & 20.
Kiini cha kampeni hizi ni Raisi wa shirikisho la soka Nchini humo (FUFA) ambaye aliingia madarakani mwaka 2013 akimshinda Lawrence Mulindwa aliyekua Raisi awali kwa zaidi ya asilimia 93 ya Kura. Hakuna aliyesita kumpa kura Moses Hasim Magogo, kwani kabla ya kua hapo huko awali alikua kwenye nafasi mbalimbali ikiwemo Makamu wa Raisi wa FUFA.
MABADIRIKO chini ya Magogo.
Shirikisho la soka Uganda (FUFA) chini ya Magogo limefanya mabadiriko mengi Sambamba na kuanzisha ligi ya vijana 2015 ambayo hapo awali haikuwepo, Hii ilikua ni moja ya Sera zake. Kwa sasa Uganda Kuna ligi ya Vijana chini ya Miaka 15-19 inayodhaminiwa na Airtle kwa mkataba wa Milioni 55 za Kiganda FUFA Junior Cup, ambayo ndio imetoa wachezaji wote katika kikosi cha Uganda U17 (The Cubs ). na U20 (The Hippos ). Ligi hiyo inaendeshwa kwa makundi mawili Kundi A linaitwa 'Treble' kundi B linaitwa 'Hat trick'. Bingwa wa Kila kundi anacheza fainali.
TIMU ZA TAIFA. Mwaka huu (2019) Kuna mabadiriko makubwa ya kiufundi yamefanyika, hapo awali U17 na U20 kila moja ilikua na kocha wake. Ambapo kwa U17 ilikua chini ya Peter Onen (aliyechukua ubingwa wa Cecafa zonal V afcon qualify) mwaka jana hapa Tanzania baada ya kuifunga Ethiopia 3-1, na U20 ilikua chini ya Wasswa Bboswa. Hali hii imeonekana inaleta Ladha Tofauti katika aina ya Mpira kwenye kuwaunganisha vijana kutoka U17 -U20-23 mpaka kuifikia The Cranes.
Hivyo Mwanzoni mwa mwaka huu (2019) FUFA ikamteua kocha mpya Jackson Magera ambaye alikua kocha mkuu wa kikosi cha vijana cha KCCA ameteuliwa kuviongoza vikosi vyote yani U17 na U20, Magera anasifika kwa kucheza fainali mara mbili mfululizo za FUFA junior cup huku akipika vijana wengi wenye uwezo na msaada mkubwa kwa kikosi cha kwanza cha KCCA kama vile Allan Okello, Julius Poloto, Mustafa Kizza, Philbert Obenchan, Steven Serwadda, Herber Achaia.
Kikosi cha U23 (The Cobs) na Timu ya taifa The Cranes ) vinabaki kwa Sebastian Desabre. Lengo ni kuwavusha vijana kutoka U17 - 20-23- The Cranes.
Hapa Huwenda sisi Watanzania tunashindwa katika kuwaunganisha vijana wetu, Ambao watatumika kwenye U17 ni vigumu kuwakuta U23.
Mwisho wa mwezi wa pili Kuna michuano ya U20 cecafa itafanyika Uganda na Kikosi cha Uganda U17 ndicho kilotarajiwa kushiriki michuano hiyo kwasabau wanamichuano ya U17 Mwezi wa nne, lakini ratiba ya mwaliko wa Uturuki Huwenda ikaharibu mazingira yote, Kikosi hiko chini ya Magera kimecheza Mchezo mmoja wa kirafiki Dhidi ya Burundi U20 mjini Bujumbura kimeambulia kipigo cha 2-0.
Chukua hii haihusiani na mada, (Iddi Abdulwahid U17 kutoka ondurparaka ya Uganda wakati wowote anaweza kwenda kwenye majaribio klabu ya Cagriari ya Italy). Tuendelee kusubiri majibu ya Kelvin John na Morice Abraham.
Ule mpango mkakati wa 2008 ndio matunda yake haya 2019 kwa mara ya kwanza Uganda U17 inashiriki Afcon U17 Nchini Tanzania.
UGANDA kwanini wana idadi kubwa ya wachezaji kimataifa,? mwaka 2017 wakati Uganda inashiriki Afcon ilikua na wachezaji watatu tu wanaocheza soka la ndani. Wengine wanatoka nje ya Uganda katika ligi mbalimbali kubwa za ndani na nje ya africa. Timothy Denis alikua Kcca mpaka sasa yupo hapo. Wenzake Geoffrey Sserunkuma alikua Kcca kwasasa Napsa ya Zambia na Muhammad Shaban alikua Ondurparaka fc na sasa Raja Casablanca. Hawa ndio wale watatu wa ndani Afcon.
Siri ya wachezaji wa Kiganda wanaamini ligi Yao haina malipo mazuri hivyo hupambana kwenda kutafuta maisha nje ya Uganda na huanzia katika mataifa yasiyo na majina makubwa na baadae huongeza thamani zao. Huu ni uthubutu wao wenyewe katika soka. Mfano wa wanaume hao ni Gefrey Massa kutoka Police fc Almasry, Baroka na sasa Kucuk Kaskazini mwa Cyprus.
Wengine. Tony Maweje Kcca, URA na sasa Tirana Albania. Luagga kizito Vipers, Rio Ave ureno na sasa Bate bolisov ya Beralus. Farouk Miya Vipers, Standard Liege na sasa Gorica ya Croatia, Denis Onyango SC villa, St George, Mamelod sundown SA. Muhammad Shaban Vipers, Raja casablanca ya Morocco. Joseph Ochaya Kcca Asante kotoko na sasa TP mazembe. Khalid Aucho, Jinja municipal, simba sc, Gor mahia na sasa Churchill Brothers fc ya India. Salim Jamal, Express fc, AL mereikh na sasa AL Hilal ya Sudan. Hawa ni mfano tu.
Wadau wengi wa soka Nchini Tanzania wanaichukulia TFF kama moja ya taasisi zinazoonekana kurudisha soka nyuma, Uganda wanachukulia FUFA kama taasisi ya Malaika iliyokuja kukomboa soka Lao na Moses Magogo ambaye ndio Rais amepokea zawadi ya Mganda bora katika ushawishi wa taifa Lao, Tuzo ambayo kama Tanzania ingekuwepo sidhani kama ingekwenda kwa mheshimiwa Raisi wa Taasisi yetu.
Siku chache zilizopita Shirikisho la soka Tanzania likiomba wadau wajitokeze kama mawakala wa soka, pale Uganda FUFA ya Magogo kupitia mkutano wa 64 wa FIFA uliofanya Juni 24 2014 mjini Sao Paulo Umepitisha mafunzo ya uwakala wa Wachezaji kwa muda wa miaka miwili kwa tiketi ya FIFA huku mawakala lukuki wakianza kazi rasmi uganda, Lengo kuu ni kuwatafutia wachezaji maisha nje ya Uganda Sambamba na kuwatoa vijana wa U17 na U20 kwenda kucheza soka la kulipwa.
Chukua hiyo (Peter Onen ambaye alikua kocha wa U17 ya Uganda baada ya Mchezo wa fainali Dhidi ya Ethiopia alisema Kuna wachezaji 7 wa kikosi chake wapo nje katika majaribio katika mataifa mbalimbali ). Hivyo hakua nao. Umejifunza nini ?
Taifa stars mpaka sasa haina imani kama Uganda inaweza kuwa njia ya wao kufuzu Afcon 2019 Egypt, Uganda Hana cha kupoteza na wanaonekana wana ubavu wa kupambana na taifa lolote Africa, hawakufika pale kwa kubahatisha. Nakukumbushia wanashika nafasi ya 70 katika viwango vya FIFA vilivyotoka January 2019. Tuendelee kusubiri huruma Yao ikishindikana tuwasome.
Ule msemo wa mwanzo wa makala haya unatafsiriwa ivi
" Nafasi ya kujifunza ni zawadi, Uwezo wa kujifunza ni utashi, uhitaji wa kujifunza ni chaguo "
Gharib Mzinga.
Chuo kikuu cha uandishi wa habari, Udsm.
0719332155.

No comments