UKWELI USIOSEMWA MATOKEO MABAYA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2018 MIKOA YA KUSINI (LINDI, MTWARA NA RUVUMA)
Anaandika: Mwalimu Bakari Madaya
Salaam Wanakusini wenzangu!
Kwamba, nami naomba kutumia fursa hii ili kutekeleza Uhuru wa kikatiba wa kutoa maoni na kuongea kuhusu masuala mbalimbali ya Kinchi. Leo hapa hususani ni Kuhusu Matokeo duni katika kanda yetu Kusini.
Kwamba, tunapozungumzia matokeo hafifu; zaidi tunazungumzia matokeo ya Sekondari. Kwamba Sekondari zetu hazifanyi vizuri karibu kila mwaka.
KUWA, Mimi nikiri hapa kwamba, uduni wa matokeo yetu hauwezi ukawa na sababu moja. Lahasha, bali ni mchanganyiko wa sababu nyingi.
Kwamba, kwangu mimi, nyingi ya sababu hizo naziona na minor kwani hata webzetu wanazo changamoto kama Zetu lakini bado hawazungumzii matokeo duni katika Mikoa yao.
Kwamba, tunapozungumza matokeo duni, tunazungumza kwa uduni wa matokeo yenyewe unaotokana na msingi wa kujilinganisha na wengine.
Kwamba, Mimi binafsi siamini sana sababu za kimiundombinu, vitabu, motisha, mishahara midogo au mazingira duni ya kufanyia kazi.
Kwamba, msingi wa kutoamini hivyo ni kwasababu tu kuwa, mishahara ya walimu wa sekondari zote unafana, mazingira ya kujifunzia yanafanna hasa katika shule za Kata, motisha hakuna kwa walimu wa Moshi, Pwani, Daresalaam au kokote nchini. Miundombinu inafanana kote nchini. Tunavyolia sisi kuhusu uhaba wa Vitabu; wenzetu nao wanalia lakini katika mazingira hayohayo yanayofanana bado wenzetu wanatuacha sana.
Mimi siamini pia kama kuna walimu hawaajibiki, wengine wanasema hapa kwamba Wakuu wa shule wamekosa managerial Skills. Jamani hii siyo kweli hata kidogo.
Mimi ninayeongea hapa ni Mwalimu, halafu nimefundisha mikoa mingi ikiwemo hiyo ya kusini. Mimi nakiri hapa kuwa Viongozi wa Kusini wanahuzunishwa na kukerwa sana na matokeo haya hafifu.
Kwamfano Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Gelacious Byakanwa anapata usingizi kidogo ila kuwaza Elimu, Inafika wakati anaandaa mikakati ya kuinua ufaulu Mkoani Mtwara, anaita wadau wa elimu Mara kadhaa kujadili namna ya kuinua ufaulu, anatoa adhabu kwa halmashauri inayofanya vibaya, adhabu ya vinyago. Alitoa maagizo ya kuandaliwa kwa mbao za matangazo na kuwabandika walimu waliofaulisha zaidi na wanafunzi walioongoza ufaulu katika kila shule ili hatimaye kuwapa hamasa wengine kuingia kwenye mbao za matangazo.
Yapo Mengi yanayofanywa MARAC kusini kuinua Elimu lakini bado juhudi hizi hazizai matunda katika shule za sekondari na zinazaa matunda katika shule za msingi Kwanini?
Afisa Elimu Mkoa, wakuu wa wilaya, Maafisa Elimu Sekondari Wilaya wanaitisha vikao Mara kadhaa tu na Wakuu wa shule na Waratibu, watendaji Kata na makatibu tarafa kuwapa maelekezo na kujadili namna ya kufanya kuinua ufaulu lakini bado tunashindwa na wenzetu Kwanini?
Huku kusini, kuna kitu kimeanzishwa kinaitwa Kambi maalum kwa watahiniwa wa mitihani. Katika hizo kambi, watoto wanafundishwa na kusimamiwa vilivyo. Wanaanza masomo SAA 12:30 na wanafundishwa tena na/ kusimamiwa Group Discussion wakati wa Jioni saa 10 hadi 12. Wanaingia Prep. SAA 2 hadi saa 4:30 usiku huku walimu wakisimamia usomaji. Katika hizo kambi Wakuu wa shule na Walimu wao huaamsha wanafunzi saa 10:30 Alfajiri kwa ajili ya jogging kidogo na kisha 10:30 hadi 11:30 darasani kujiisomea na kusimamiwa.
Kwenye hizo kambi, jmamosi na jmapili watoto wanasoma na kusimamiwa na kufundishwa na Walimu. Nenda katika halmashauri ya wilaya ya TANDAHIMBA utayaona hayo, licha ya juhudi zote bado wenzetu wanatuacha. Kwann?
Ikumbukwe kwamba, STANDING ORDERS FOR THE PUBLIC SERVICE 2009 inawataka watumishi wa serikali kufanya kazi kwa kuanzia 1:30 hadi 9:30 na kwamba kama italazimika mtumishi kufanya kazi kwa muda wa ziada basi mwajiri atamlipa mwajiriwa wake kwa muda huo ziada. Lakini Tazama wilayani Tandahimba kwa mfano walimu wanafanya kazi hizo tena bila kutaraji chochote. Wanafanya hivyo kwasababu tu na wao wanaichukia hali hii. Walimu wanajitoa sana lakini bado matokeo yanakuwa hafifu kwanini?
Ningeweza kuandika hapa jitihada zinazofanywa na walimu katika mikoa ya kusini lakini ngoja niishie hapa, niende kwenye hoja sasa.
Kwanza mimi nakiri kabisa kuna tatizo lipo tena kubwa tu ambalo linasababisha matakeo hafifu katika mikoa yetu. Sijafahamu kwanini haliongelewi.
Kwamba, kabla ya kuwalaumu Wadau wa elimu ya sekondari na kabla ya kuanza kuleta mbinu za kufaulisha kwa sekondari; ni vema tukaangalia chanzo kikuu cha matokeo duni.
Kwamba, ni vema tukajiuliza maswali kwamba, wanafunzi hawa waliotusababishia kuingia mwishoni kitaifa; matokeo yao ya darasa la saba yalikuwaje?
Je katika matokeo ya darasa LA saba ya mwaka 2014 na 2016 yalikuwaje? Je tulikuwa wa mwisho?
Je kama hatukuwa wa mwisho, kwanini sekondari tumekuwa wa mwisho?
Au wanafunzi Hawa na Wazazi na walezi wao walikuwa na mwamko was elimu shule za msingi lakini mwamko huo ukayeyuka walipofika sekondari?
Au wanafunzi hao walikuwa na magenious kule primary na akili zao zikayeyuka walipokuja tu sekondari?
Au Walimu wa shule za msingi wapo Competent zaidi kuliko wa sekondari? Au wao walisoma vyuo tofauti na vile vilivyopo Tanzania
Au Kuna miundombinu bora katika shule za msingi kuliko sekondari?
Au shule za msingi kuna VITABU vya kutosha kuliko sekondari. No!
Au walimu wa shule za msingi wanapata motisha na mishahara mikubwa kuliko sekondari?
Au walimu wa msingi wanafundisha zaidi kuliko vile nilivyoeleza kwa walimu wa sekondari?
SASA jiulize katika hilo jibu ulilopata kwanini wanafunzi walewale wasiwe wa mwisho darasa la saba na wawe wa mwisho sekondari ilihali wanafunzi walioshindanana nao ni walewale? Shida inaanzia hapo jamani
Kuna mwalimu Fulani huko nyumbani kusini aliniambia kuwa, katika shule yao waliwapa wanafunzi wa kidato cha kwanza mtihani wa Imla na hatimaye waliwabaini wanafunzi 8 ambao hawakujua kusoma na kuandika na karibia wanafunzi 15 waljua kusoma na kuandika na wawili kati yao waliandika kwa shida majina yao. Anasema mmoja wao aliandika jina lililosomeka "A b. DA. Ra" akimaanisha "Abdallah"
Wanafunzi hao waliendelea kusoma sekondari. Sasa watoto kama hao wanafanya mitihani ya sekondari wanafunzi 70 darasani. Kati yao tayari kuna zero za mapema kama 23 hivi. Unategemea ushindane na wenzako ambao angalau wamefanya "mishe" hatimaye "kufaulisha wanafunzi wanaojiweza" Amesema nani?
Kwangu mimi hiyo naiweka sababu kubwa inayosababisha matokeo hafifu.
Sababu ya pili ni utayari wa wanafunzi wenyewe. Unaona hapo kwamba kule TANDAHIMBA hakuna shule ambayo hawakai kambi na nimeeleza namna wanavyosoma kupitia program ya kambi. Kule Tunduru karibu shule zote za Kata zimefanywa kama za bweni kwa mtindo wa wanafunzi wote kuchangia chakukula na kuishi shuleni wakati wote lakini bado kuna shule ya Mbesa sekondari ilikuwa ya mwisho matokeo ya 2017. Shida nnyingine ni utayari wa wanafunzi wenyewe.
Kwangu mimi kukaa kambi hasadii endapo wanafunzi wenyewe hawajawa tayari kutoka miyoni mwao kubadilika na kupenda Elimu kwa dhati kabisa kutoka moyoni. Kambi haiwezi kufua dafu katika hali hii.
Juhudizmaafis elimu na watekelezaji wa mitaala hazitakuwa na athari endapo wanafunzi hawajawa tayari na hawwjadhamiria kutoka miyoni mwao.
Kama Wanafunzi hawapo tayari, watafika shule na watatekeleza shughuli za ujifunzaji kwa kuigiza tu.
Watajifanya wameshika madaftari kwa kuwa tu Headmaster amesema, kwakuwa tu walimu wamesema. Siyo kwakuwa huu ni wajibu, niutekeleze ili hatimaye nifanikiwe. Hawatafanya hivyo
Kama wanafunzj hawajawa tayari katika kusoma; maana yake watakuwa wanatia kelele darasani lakini wakimuona tu Mwalimu anapita basi watajiganya kimya huku wakijidai kuandika Summary kwenye vijikaratasi kukudanganya wewe wapo busy kusoma, kumbe wapi wanakuogopa tu. Miyoni mwao wanawaza mengine kabisa.
Kuna wakati utaona shule ipo kimya. Na mgeni akija au hata wewe mwenyewe utasema sasa somo limeeleweka. Kumbe wapi wanaogopa walimu tu. Hawasomi. Hii yote inayotokea kwasababu tu ya mioyo yao kutokuwa tayari kusoma.
Kuna wakati nilikuwa Prep nasimamia. Niliwakuta wanafunzi wapo busy. Nikajisemea ahsante Mungu sasa kizazi kinaelewa. Subutu!
Nikamwita pembeni mwanafunzi mmoja nikamuuliza ulikuwa unasoma kitu gani? Nilimuuliza huku nikijua kuwa alikuwa anasoma nini. Akanijibu. Nikamuiliza aniambie definition ya kitu kile. Alishindwa. Nilihisi labda kwa hofu ya kuongea, hivyo nikamwambia basi aniandikie sehemu, mimi nikatoka kidogo ili nimpe nafasi ya yeye kuandika.
Kwamba, Niliporudi alikuwa bado hajaandika. Nikamuuliza sasa ni saa 4 usiku. Je kuna kitu kingine umesoma zaidi ya hiyo definition? Akasema hakuna. Aisee nikachoka. Nilimwambia kesho anione ofisini. Niligundua vingi sana baada ya kuongeanaye.
Hii ndo sababu ya kwanini matokeo yetu ni hafifu licha ya jitihada kubwa zinazofanywa.
Wanafunzi wetu hawapo tayari. Hii ni kubwa na ya msingi sana. Wanaenda shule kwasababu ni utaratibu wa nchi yetu. Hawaufanyi huo kama wajibu wao kwanza.
Kwahiyo, utaona hapo kwamba wapo wanafunzi wale wenzangu na mimi (wasioweza kusoma na kuandika pamoja na wanaosoma kwa shida).
Sababu ya Tatu ni utoro. Utoro huu unasababishwa na kukosekana utayari. Hivyo hapa itakuwa kama ni Minor point, lakini nitaielezea hapa kutokana athari yake kuwa kubwa.
Kwamba, naomba ifahamike hapa kwamba, wapo wanafunzi wanafika shuleni kila siku lakini mioyo yao haipo shule. Wamejudhuria tu huenda kwasababu Wazazi wake ni wakali au ameenda shule ili tu kukutana na kampani yake huko shuleni. Hatoki nyumbani kwa kuahadi nafsi yake kwamba Leo lazima nikajue jambo Fulani na lazima jambo hilo likakae kichwani. Hawafanyi hivyo lakini kila siku wanahudhuria. Hawa nao hawapo tayari. Wanafanya mitihani ya taifa kisha wanafeli.
SASA kuna hili kundi lingine la watoro. Hii ni sababu ya matokeo duni huko Kusini.
Utaratibu wa kumuondoa shuleni kwa utoro, hadi pale atakapotoroka siku 90 mfululizo. Sasa wanafunzi siku hizi wanajua hilo. Wanachokifanya wao ni kutoraka siku 80,halafu anakuja tena wiki moja hadi mbili hivi kisha anatoweka tena.
Atavizia hivyo kisha baadaye utamuona anatokeza kwenye mitihani. Na yeye anataka kufanya mtihani. Aisee! hatari sana. Anafanya na hivyo anaongeza idadi ya failures. Kusini hatimaye inakuwa ya mwisho. Inasikitisha sana.
Wapo wapo wanafunzi ambao wanakuwa na mahudhurio ya siku 60 kwa mwaka kisha wanafanya mtihani wa Taifa. Anafanya mtihani sawa na yule wa Kilimanjaro aliyehudhuria masomo kwa siku 190 kati ya 195 za masomo kwa mwaka. Kwa hali hii tutashindana kweli?
Kule Naputa Sekondari-Tandahimba, kuna taarifa nikisoma somewhere kwamba matokeo ya kidato cha pili walifeli wanafinzj 19 kati ya hao 15 walikuwa na tabia ya utoro. Unaiona hiyo? Utoro unaturudisha nyuma sana.
Kwamba sasa naomba nijikite kwenye suluhisho ya nini kifanyike:-
Mosi, jambo kubwa ambalo wanakusini na viongozi wake wajikite nalo ni kujenga utayari wa wanafunzi na Wazazi.
Jambo hili litiliwe mkazo sana tena sana sana. Iwe ni wimbo huu. Uimbwe sehemu zote. Kila Kona, kila kijiwe izungimzwe elimu kwa angalau 30 ya maongezi yote ya sehemu husika.
Katika kutekeleza hili kupandikizwe watu vijiweni, mikahawani na sehemu zingine wanazopatikana watu ambao kazi yao kubwa iwe ni kuhakikisha ajenda ya elimu inachukuwa nafasi kuliko chochote. Watu Hawa wawe mahiri wa kuongea kuliko hao watakaokuwa vijiweni na wawe na ushawishi mkubwa.
Walimu wahakikishe kila kipindi angalau dakika 3 watumie kujenga utayari kwa wanafunzi kupenda kusoma. Mashuleni kuwekwe siku maalumu itakayoitwa siku ya Elimu au vyovyote ambapo walimu na Bodi za shule ziongee na wanafunzi kuhusu kwanini wanafunzi walirithi Elimu na siyo mikorosho.
Aidha, kutengwe siku moja ya kila mwenzi wa 12 au wa kwanza kabla ya kufungua shule ambayo pia good orators waandalie kuwasilisha mada no kwanini jamii ilirithishe Elimu na siyo Mashamba.
Suluhisho la pili ni kumfanya kila mwanajamii kuwajibika kwa kila mwanafunzi kupata elimu.
Jamii ihakikishe kwamba, wanafunzi wote wanaenda shuleni bila kujali huyu ndugu yangu wa damu au vinginevyo.÷÷44
Kila mwanajamii awe na haki ya kukamata watoro mtaani na kuwapeleka shule na kwamba mtu atakayekataa au kutia ugumu katika aonekane kama mhaini. Asivumiliwe asilani. Awekwe Lupango.
Ifike wakati wacheza pool wawaone wanafunzi wanaokuwa nao kwenye pool kama balaa inawafuata. Wasikubali kuwa na mwanafunzi club, pool,draft, kamari. Na serious measures zichukuliwe dhidi ya watu watakaowavumilia wanafunzi katika maeneo yao.
Ifike wakati wanafunzi waonwe kama wezi wanapokuwa mtaani wakati wa masomo. Ihubiriwe na kufanyika hivyo kwa dhati kabisa.
Ifike wakati mwanafunzi naye aogope kukutana na RAIA yeyote mtaani wakati masomo. Mwanafunzi amuone RAIA kama balaa linamjia mbele yake. Yakifanyika hayo hakuna utoro kusini.
Namalizia kwa kusema kwamba hakuna linaloshindikana kukiwa na dhamira ya dhati kwa maana tukiwa na dhamira ya dhati tutamtanguliza Mungu ili kufanikiwa haya.
AHSANTENI SANA.
No comments