YASSER IBRAHIM AREJEA KUWAKABILI SIMBA.
Kocha wa Al Ahly, Martin Lasarte ametangaza majina 21 ya wachezaji wake watakaosafiri kuja Tanzania kuwakabili Simba SC kwenye klabu bingwa Afrika hatua ya makundi.
Simba watawakaribisha Al Ahly uwanja wa Taifa Tanzania siku ya Jumanne, Februari 12 baada ya Al Ahly kuwafunga Simba bao 5-0 kwenye uwanja wa Borg El-Arab wiki iliyopita.
Al Ahly wanaongoza kundi wakiwa na alama saba (7), wakiwazidi AS Vita Club kwa alama tatu ambao wao wana alama nne, wakiwazidi pia Simba wanaoshika nafasi ya tatu kwa alama 4 wakiwa na alama 3, wakati JS Souara wanashika mkia kwenye kundi wakiwa na alama 2.
Pia timu imeongezwa ngumu kwa kurejea kwa beki wao Yasser Ibrahim baada ya kukosa michezo mitatu iliyopita kwa sababu ya majeruhi, pia Mohamed Sherif anarejea kikosini.
Kwa upande mwingine, nahodha wa timu Hossam Ashour atakosa mchezo huo kwa sababu ya majeruhi pamoja na Walid Azaro, Ahmed Fathi, Walid Soliman, na Marwan Mohsen.
Kikosi Kamili:
Magolikipa: Sherif Ekramy, Mohamed El Shennawy, na Ali Lotfi.
Mabeki: Saad Samir, Rami Rabia, Ayman Ashraf, Ali Maaloul, Mahmoud Wahid, Mohamed Hany, Yasser Ibrahim.
Viungo: Amr El-Sulya, Karim Nedved, Hamdi Fathi, Islam Mohareb, Hussein El-Shahat, Ramadan Sobhi, Nasser Maher, Mohamed Sherif, Hesham Mohamed.
Washambuliaji: Salah Mohsen, Junior Ajayi.

No comments