Breaking News

" Hatutaki mgombea wa Urais" - Polepole



Baada ya Chama Cha Mapinduzi kumpokea aliyekuwa mgombea urais wa CHADEMA kwa mwamvuli wa Ukawa, Edward Lowassa mwishoni wa wiki hii, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole amesema si kwa sababu ya nafasi ya kugombea.

Akijibu maswali pamoja na maoni ya wafuasi wake katika ukurasa wake wa twitter, Polepole amesema kwamba chama hicho kitaendelea kusimamia kanuni na kuwa hazitabadilika.

Kanuni daima zitabaki kuwa kanuni na hazitabadilika, lakini wakati huu hali ni tofauti . Hatutaki mgombea wa urais. Mtu ameomba nafasi ya uanachama, we are a mass party but very keen as to who becomes our leader jana, leo na kesho!".

Hivi karibuni Edward Lowassa aliyekuwa mgombea wa urais mwaka 2015 kupitia UKAWA, alitimkia CCM huku akisema kwamba amerejea nyumbani.

Hata hivyo sehemu mbalimbali, Polepole amekuwa akifafanua kwamba kwa sasa CCM Lowasa ni mwanachama wa kawaida kabisa.

No comments