RC Mghwira awataka wafanyabiashara wa Kilimanjaro kuchangamkia fursa za Benki ya CRDB.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amewataka wafanyabishara wa mkoa huo kuchangamkia fursa za kibiashara zinazopatikana ndani ya Benki ya CRDB ili kuboresha tija na ufanisi wa biashara zao na kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli katika dhana yake ya kujenga Tanzania ya viwanda.
Mama Mghwira aliyasema hayo alipokuwa akifungua rasmi semina ya wafanyabishara wa Mkoa wa Kilimanjaro iliyofanyika katika ukumbi wa Kuringe mjini Moshi. Semina hiyo ilijumuisha wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka nyanja tofauti, ili kuwaonyesha fursa mbalimbali zilizomo ndani ya Benki ya CRDB zitakazowawezesha kuongeza mitaji, kupata mikopo pamoja na ushauri wa kitaalamu ili kuongeza ufanisi wa biashara zao.
Alisema kuwa pamoja na lengo la kubwa la Benki ya CRDB kuandaa semina hiyo ya wafanyabiashara na wajasiliamali ili waweze kukua na Kukopesheka na kuboresha biashara zao, bado jukumu la kutumia fursa hizo linabaki mikononi mwa wafanyabishara hao.
Alisema kuwa Serikali kushirikiana na wadau kama Benki ya CRDB wana nia thabiti ya kujenga mazingira ya kuwawezesha wafanyabishara kupata mitaji ili kuongeza ukuzaji wa uchumi. Alisema kuwa kwa ubunifu ulionyeshwa na benki ya CRDB katika kuwainua wafanyabishara unaonyesha ni kwa kiasi gani Benki ya CRDB inasapoti kwa vitendo juhudi za serikali katika kujenga uchumi endelevu na wenye kugusa sekta zote za uzalishaji.
Kwa upande wa wafanyabishara wadogo maarufu kama wamachinga, Mheshimiwa Mghwira aliitaka Benki ya CRDB kuendelea kuwa wabunifu na kuleta bidhaa kwa ajili ya kundi la wateja wadogo yaani wamachinga ambao wana mchango mkubwa katika uchumi wa taifa. “Serikali imeanza kwa kutoa vitambulisho kwa wajasiliamari ili kuwarasimisha, hivyo Benki zina kujukumu la kwenda mbele zaidi kwa kuwapatia mikopo nafuu ili waweze kukuza baishara zao” alisema mheshimiwa Mughwila.
Akizungumza katika warsha hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela, alisema “Hakuna biashara inayofanikiwa bila kuongeza mitaji na kuzikabili changamoto zake. Lengo kuu la Benki ya CRDB ni kuwafungulia fursa nyingi zinazoweza kuendeleza biashara zao.
Mbali na kufaidika na ujuzi wa mambo kupitia semina hii, wafanyabiashara pia watafaidika kwa kujenga uhusiano wa kibiashara baina yao na hivyo kuongeza ujuzi wa kibiashara na kupanua wigo na masoko ya biashara zao” alisema.
Nsekela alisema kuwa Benki ya CRDB inatambua umuhimu wa wafanyabiashara katika kukuza uchumi wa nchi lakini pia inatambua kwamba uchumi hautakuwa kama wafanyabiashara hao hawatakuwa na nyenzo sahihi za kibiashara.
“Nichukue fursa hii kuwahakikishia wafanyabishara wa mkoa wa Kilimanjaro kuwa Benki ya CRDB imejipanga vyema katika kufikia matarajio yao yote ya kibenki.
“Huduma zetu zinakidhi mahitaji ya makundi yote ya jamii kuanzia watoto, wakubwa, kinamama, wafanyabishara wadogo, wakati na wakubwa. Pia tunafanya biashara za Bima na kukusanya malipo yote ya serikali kuanzia malipo ya ankara, kodi na mengineyo. Pia Benki inawahudumia wateja wadogowadogo kupitia kitengo chake cha wajasiliamari yaani CRDB Bank Microfinace” alisema Nsekela.
Semina ya Benki ya CRDB kwa wafanyabishara wa mkoa wa Kilimanjaro ni sehemu ya mipango mkakati wa Benki hiyo wa kuwafikia wateja wake ilik kuwaainishia huduma mbalimbali zinazopatikana ndani ya benki ya CRDB. Benki pia imeshafanya semina kama hizo kwenye mikoa ya Mwanza, Arusha, Iringa na Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira akizungumza wakati alipokuwa akifungua rasmi semina ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Kilimanjaro iliyoandaliwa na Benki ya CRDB ambayo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Kuringe mjini Moshi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza wakati wa semina ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Kilimanjaro iliyoandaliwa na Benki ya CRDB ambayo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Kuringe mjini Moshi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay akizungumza wakati wa semina ya wafanyabiashara wa Mkoa wa Kilimanjaro iliyoandaliwa na Benki ya CRDB ambayo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Kuringe mjini Moshi.
No comments