Breaking News

Bilionea Mo Dewji akumbushia jambo Simba SC baada ya miaka 18



Mfanyabiashara maarufu nchini na muwekezaji ndani ya Simba SC, Mohammed Dewji amesema kuwa mafanikio waliyapati timu hiyo mwaka 2003 katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika ni kitu ambacho kitabaki kuwa histori  kwao siku zote.

Kauli hiyo inakuja wakati timu hiyo ikiwa na khari ya hali ya juu kabisa kuhakikisha wanatwa taji hilo kwa mara ya kwanza.

"Mafinikio tuliyoyapata kwa kipindi kile (2003) kuwa timu ya kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki na kati kuifunga klabu bingwa ya wakati huo ya Afrika Zamalek ya Misri. Na ushindi huo unabaki kuwa moja ya mafanikio makubwa katika historia ya klabu yetu," ameeleza Mo Dewji.


Keho Jumamosi Simba SC itacheza mechi yake ya pili ya Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika mjini Kinshasa dhidi ya wenyeji, AS Vita ambao mechi yao ya kwanza walifungwa 2-0 na wenyeji, Al Ahly nchini Misri.

No comments