CCM siyo chama cha kutetereka tena - Dkt. Bashiru
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amesema kupitia mfumo wa vyama vingi chama hicho kimeweza kuimarika zaidi na kufanya mabadiliko mengi ndani ya chama na hata kwa wanachama.
Alibainisha hayo Dodoma wakati akifungua mjadala wa wana CCM wa Mkoa wa Dodoma pamoja na wadau mbalimbali kujadili mapendekezo ya muswada wa Sheria ya Vyama vya siasa .
“Kupitia mfumo huu wa vyama vingi kumekuwa na ushindani mkubwa miongoni mwa vyama na hata ndani ya chama”alisema Dkt. Bashiru.
Hata hivyo amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa vyama vingi bado kunahitajika kuwepo kwa vyama ambavyo vitalinda umoja, amani na utulivu wa nchini.
Aliendelea kwa kusema, 'CCM siyo chama cha kutetereka tena kwani hivi sasa ni mashambulizi tu hakuna sababu ya kubabaika malengo waliotuachia waasisi wetu ya kulinda amani na utulivu ndiyo tunayo yasimamia'.
No comments