Kesi Ya Wambura Na TFF Yachukua Sura Mpyaa FIFA Waingilia Kati.
Shirikisho la soka duniani (FIFA) kupitia kitengo cha Sheria January 14 mwaka huu limeiandikia barua shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kutaka maelezo ya kina kuhusu kufungiwa kwa makamu wa Rais wa shirikisho hilo Bwn. Michael Richard Wambura.
Michel Richard Wambura alifungiwa na kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mkutojihusisha na masuala ya soka maisha ila Wambura alienda mahakamani kuomba Review ya hukumu yake na mahakama ikamrejesha madarakani kutokana na kamati ya Maadili iliyokuwa ikiongozwa na Marehemu Hamidu Mbwezeleni kutoa hukumu bila kufuata sheria.
Pia Makamu wa Rais na Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Mara (FAM) Michael Richard Wambura alituma malalamiko yake FIFA kutokana na anachofanyiwa na shirikisho la soka Tanzania (TFF) ndio maana shirikisho la soka Tanzania limeombwa kupeleka maelezo ya kina kuhusu kufungiwa Wambura. Tangu January 14, 2019 mpaka jana January 17 shirikisho la soka Tanzania halijaijibu barua hiyo.
No comments