Breaking News

Ratiba Ya Klabu Bingwa Afrika Wiki Hii, Leo Na Kesho Hapatoshi.


Michuano ya klabu bingwa Afrika hatua ya makundi itaendelea wiki hii kwa michezo ya raundi ya pili kwa kila kundi.

Leo Ijumaa michezo kadhaa itapigwa katika viwanja mbalimbali vya mataifa tofauti.

Ismaily SC wao watakuwa katika dimba lao la nyumbani kuwaalika Club Africain huku Orlando Pirates wakiwa pale bondeni kwa madiba kuwakaribisha  Horoya AC  nao
Esperance ya Tunisia wao watakua wenyeji wa FC Platinum huku timu inayotajwa kuwa kibonde kwenyekundi D JS Saoura ya Algeria wao watakua nyumbani kwao kuwaalika Al Ahly SC kutoka Misiri


Aidhi kipute kitaendelea kwa kesho jumamosi kwa wawakilishi wa Tanzania Simba sc kuwa wageni wa AS Vita Club mchezo utakaopigwa mjini Kinshansa. ASEC Mimosas wao watakuwa wenyeji wa Lobi Stars huku CS Constantine  waliwaalika wababe TP Mazembe
Mamelody Sundowns wao watakua na kibarua kigumu dhidi ya  Wydad Casablanca

No comments