Mume wa Malkia wa Uingereza Philip, Duke of Edinburgh amepata ajali ya gari.
Prince Phillip mwenye miaka 97 ni mjukuu wa aliyekuwa mfalme wa Ugiriki na Denmark mfalme George I.
Prince Philip baada ya kupata ajali hiyo hakuumia. Ajali hiyo imetokana na magari mawili kugonga huko Sandringham ambapo alikuwako huko na mkewe Malkia Elizabeth kwa ajili ya likizo za sikukuu ya Krismasi.
Hata hivyo Prince Philip aliacha kutumia majukumu ya kifalme mwaka 2017. Prince Philip na Malkia walioana tokea mwaka 1947.
No comments