MAKALA: SIMBA IJIFUNZE KWA ENYIMBA WA 2003
Mwaka 2003, Simba ilitinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ikaangukia kundi A sambamba na Enyimba International kutoka Nigeria, Ismailia kutoka Misri na Asec kutoka Ivory Coast.
Kundi hili ndilo lililokuja kutoa timu zilizocheza fainali na hatimaye timu moja kuwa bingwa. Timu hizo ni Enyimba International (ikawa Bingwa), na Ismailia.
SOMO KUTOKA ENYIMBA
Simba inaweza kujifunza kitu kikubwa sana kutoka kwa Enyimba ambao waliibuka Mabingwa wa Afrika mwaka huo.
Miamba hao kutoka Nigeria, walianza kwa ushindi wa nyumbani wa 3-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa kwanza, lakini katika mchezo wa pili, wakafungwa 6-1 na Ismailia.
Kipigo hiki kiliwashtua sana na kuwafanya wayaone mapungufu yao na kujipanga kuyafanya kazi.
Na kweli, walijipanga vizuri, wakianza na Asec waliyoifunga 3-1 nyumbani 2-0 ugenini.
Hadi wanakuja Dar Es Salaam kurudiana na Simba, tayari walikuwa na alama 9 safi.
Wakapoteza 2-1 dhidi ya Simba jijini Dar Es Salaam lakini waliporudi kwao kurudiana na Ismailia, kwao, wakawafunga 4-2 na kutinga nusu fainali.
Kilichowasaidia Enyimba ni kushinda mechi zao zote za nyumbani, walipochanganya na ushindi mmoja wa ugenini dhidi ya vibonde, Asec, wakaongoza kundi.
Wao na Ismailia wakakutana tena kwenye fainali ambako kila timu ilishinda nyumbani lakini ushindi wa Enyimba ulikuwa mkubwa zaidi na kuwasaidia kuwa mabingwa. Walishinda nyumbani 2-0, wakafungwa ugenini 1-0.
Endapo Simba itapita njia za Enyimba , hakuna atakayekumbuka kipigo cha 5-0 na badala yake tutakukuwa tunangumzia mafanikio yakatayofikiwa.
Zaka Zakaz

No comments