Breaking News

Masoud Djuma Afunguka Haya Baada Ya Simba Kupigwa 5-0

-Kipigo cha mabao 5-0 ilichokipata Simba katika ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita ya Congo kimemfanya kocha aliyewahi kuinoa klabu hiyo Mrundi Masoud Juma kuvunja ukimya huku akimpa akili bosi wake wa zamani Patrick Aussems.

-Masoud aliyekuwa kipenzi cha mashabiki, kabla ya kuvunjiwa mkataba wake ikidaiwa kuwa anaigawa timu alisema Simba inatakiwa kuwa na heshima kubwa inapocheza ugenini kwani wakienda na mbinu ya kushambulia hawatapata hata alama moja kwa kuwa timu wanazocheza nazo zina uwezo mkubwa.

"Kwanza wanatakiwa kuwa na mahesabu makali ya kupata hata alama moja ugenini, kwani Simba inao uwezo wa kupata alama 9 nyumbani wakifanya hivyo watamaliza kundi wakiwa na angalau alama 10 na kufuzu robo fainali"

"Lakini wakisema washinde mechi zote za nyumbani bila wao kupata hata alama moja ugenini itakuwa ni bure. AS Vita na Al Ahly ni timu kubwa barani Afrika na inapaswa kuwapa heshima unapocheza nazo nyumbani kwao vinginevyo utaadhibiwa vikali.."

Alisema Irambona Masoud Djuma

No comments