Sina cha kuhofia kwa mpenzi wangu – Beka Flavour
Msanii wa muziki Bongo, Beka Flavour amesema kuwa mara kadhaa amekuwa akiweka picha za mpenzi wake kwenye mtandao na haofii chochote kwani wanaaminiana.
Muimbaji huyo amefunguka hayo akipiga stori na Clouds FM ambapo amesema hata hasipo muweka mtandaoni kama si mwaminifu haitosaidia chochote.
“Mwanamke kuchukuliwa na mwanaume mwingine kwa sababu ya kumpost kwenye mitandao ya kijamii basi huyo mwanamke hana mapenzi ya dhati kwa mwenza wake japo kuna baadhi ya watu wanamsumbua kwenye Dm yake ila kwa sababu namuamini (Tunaaminiana) hivyo sina cha kuhofia kwake” ameeleza Beka
Utakumbuka Beka Flavour aliyekuwa miongoni mwa wasanii wanaounda kundi la Yamoto Band, yeye na mpenzi wake aitwae Happiee Reuter wamejaliwa kupata mtoto mmoja kwenye mahusiano yao.
No comments