Simba yashusha wapya 2, wapiga mazoezi na Kikosi
Timu ya Simba leo 21 Janauray 2019 ilifanya mazoezi katika uwanja ambao imekuwa ikiutumia katika mazoezi ya Kila mara uwanja wa Boko Veteran uliopo jijini Dar Es Salaam.
Kikosi cha Simba kilifanya mazoezi yake kikiwa na Nyota wake takribani wote walioenda nchini Congo huku kukiwa na Ongezeko la wachezaji wawili wapya.
Wachezaji hao imeelezwa kuwa wamekuja kwaajili ya majaribio ambao ni Beki wa kati kutoka Ghana anayeitwa Lamine Moro, na Mwingine akicheza Nafasi ya Ushambuliaji Ayi Abel Kissibo.
No comments