Tetesi Za Usajili Wa Wachezaji Wa Ligi Kuu Tanzania Bara
KICHUYA HUYOOO
Klabu ya Simba imesema ipo kwenye mazungumzo ya mwisho na klabu ya Pharco ya nchini Misri kumuuza mchezaji Shiza Kichuya.
DEAL DONE AMBOKILE
Mshambuliaji wa klabu ya Mbeya City Eliud Ambokile amejiunga na klabu ya Black Leopards ya Afrika Kusini kwa mkopo wa miezi mitatu wenye kipengele cha kununuliwa moja kwa moja.
AJIBU SIWEZI KUONDOKA YANGA
"Sijui mkataba wangu umebakiza muda gani lakini siwezi kuondoka Yanga nikawaacha wachezaji wangu, nikiondoka nani atakuwa nahodha wao,"
Ibrahim Ajibu
Nahodha wa klabu ya Yanga
KAKOLANYA KUONDOKA YANGA..
Kaimu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Samwel Lukumay amesema amepokea barua kutoka kwa Mwanasheria wa Golikipa Benno Kakolanya ikisisitiza avunjiwe mkataba wake licha ya kulipwa fedha zake zote anazodai katika klabu hiyo.
No comments