Ujue Utosi wa Mtoto
Nimepata maswali na maombi mengi kutoka kwa baadhi ya wasomaji wetu wakitaka kufahamu juu ya Utosi. Baadhi ya wazazi wamekuwa na maswali mengi juu ya Utosi hasa kuhusisha utosi na imani nyingi kulingana na makabila yetu.
Je utosi ni nini?
Utosi ni nafas inayojitokeza kwenye kichwa cha mtoto baada ya mifupa miwili au zaidi inapokutana. Nafasi hii inakuwepo kwa sababu mifupa katika kichwa cha mtoto inakuwa haijafunga. Mtoto anapozaliwa ana maeneo ya namna hii sita kwenye kichwa. Wastani wa utosi kufunga ni miezi 13. Watoto wa kiume inafunga mapema zaidi kuliko wenzao wa kike.
Utosi una faida gani
Utosi una faida kuu mbili
Moja, utosi unasaidia kupunguza ukubwa wa kichwa ili kumuwezesha mtoto kupita kwa urahisi kwenye njia ya uzazi wakati wa kuzaliwa
Pili, utosi unawezesha ubongo wa mtoto kukua vizuri bila kubanwa kwenye kichwa cha mtoto.
Utosi wa kawaida ukoje?
Ngozi ya utosi inapaswa kuwa katika level moja na ngozi nyingine ya kichwa. Utosi ukivimba juu au ukizama ndani inaweza kuashiria kuwa mtoto ana umwa.
Nini husababisha utosi kuzama ndani?
Sababu kubwa inayosababisha utosi kuzama ndani ni upungufu wa maji mwilini. Hali hii inaambatana na dalili nyingine za upungufu wa maji mfano kukauka midomo, kupungua kwa mkojo na mtoto kushindwa kunyonya sawasawa.Nini husababisha utosi kuvimba?
Sababu kubwa zinazofanywa kuvimba kwa utosi ni mtoto kuwa na homa ya uti wa mgongo na kuongeza kwa presha kwenye kichwa cha mtoto. Sababu zote hizo zinaweza kuhatarisha maisha ya mtoto.
Mtoto anapolia pia utosi una weza kuvimba, lakini hurudia hali ya kawaida baada ya mtoto kunyamaza.
Je ufanye nini
Iwapo utaona hali isiyokuwa ya kawaida kwenye utosi wa mtoto, hakikisha unakwenda hali katika kituo cha afya. Daktari atampima mtoto na anaweza kukuambia tatizo ni nini. Usikae nyumbani kwa sababu mtoto anaweza kuwa na tatizo ambalo linaweza kuathiri afya yake.
No comments