Breaking News

YANGA DHIDI YA BIASHARA KOMBE LA ASFC KUPIGWA KESHO UWANJA WA TAIFA




Mchezo wa Hatua ya 32 bora wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup -ASFC) kati ya Yanga na Biashara United kupigwa Alhamisi wiki hii. Mechi hiyo ya kuingia hatua ya 16 bora utazikutanisha timu hizo katik dimba la Uwanja wa Taifa.

Kuelekea mchezo huo, makocha wamejizatiti kuhakikisha hawapotezi huku Kocha Mkuu wa Timu ya Biashara United, Amri Said amesema Yanga akiwaonya Yanga kuwa mechi hiyo haitakuwa nyepesi kwao. Said amesema kuwa kikosi chake kimejipanga kuondoka na matokeo Uwanja wa Taifa kwani anaamini wana uwezo mzuri wa kupata matokeo mbele ya Yanga.

Said amesema hana mashaka na uwezo wa wachezaji wake kutokana na maandalizi ambayo anayafanya kikubwa anachofikiria ni kupata ushindi kwenye mchezo wake na anamini dakika 90 zitaamua. “Yanga kuondoka na ushindi kwenye mechi hiyo wasifikiri ni kazi, mechi hii ni zaidi ya fainali ukiangalia zaidi ni mtoano hivyo ni lazima wachezaji waonyeshe upambanaji kwenye mchezo wetu,” amesema Said.

Said amesema, anafahamu Yanga ina timu nzuri na ni kubwa na anawafahamu na kuwaheshimu wapinzani wao ila haliwapi shaka kwani mpira unachezwa Uwanjani. Biashara United imeweka kambi katika moja ya viunga vya Jiji la Dar es Salaam wakisubiri mtanange hao baada ya kumaliza kucheza na Azam kwenye mechi ya Ligi uliomalizika kwa wao kupoteza kwa matokeo ya 2-1

No comments