Simba Yaiadhibu Mwadui Fc, Kocha Azungumzia Hali Ya Mchezo
Klabu ya Simba SC ambao ndio mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui FC ya Mkoani Shinganya.
Mchezo huo wa 15 kwa Simba na 25 kwa Mwadui ulianza majira ya saa 1:00 usiku Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam na wenyeji Simba kuibuka na ushindi huo mnono.
Mabao yaliyoipa ushindi Simba SC yamefungwa na Meddie Kagere katika dakika ya 21, Mzamiru Yassin dakika ya 26 na Nahodha wa Klabu hiyo John Raphael Bocco "Adebayor" katika dakika ya 29.
Ushindi huo unaifanya Simba isogee hadi nafasi ya 3 katika chati ya msimamo wa Ligi ikiwa na pointi 36 nyuma ya Azam Fc yenye pointi 48 na Vinara Yanga wenye pointi 55.
“Ulikuwa mchezo mgumu lakini muhimu tumepata alama tatu ambazo zimetuwezesha kuisogelea timu iliyopo mbele yetu”- Kocha Patrick Aussems baada ya ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Mwadui.
Katika mchezo mwingine wa Ligi uliopigwa lwenye Uwanja wa Mkwakwani Mjini Tanga Klabu ya Coastal ya Union ikiwa nyumbani imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Ruvu Shooting ya Pwani.
Wageni Ruvu Shooting ndio waliotangulia kufunga kupitia kwa William Patrick dakika ya 37, kabla ya Raivin Hafidhi kuisawazishia Coastal katika dakika ya 65.

No comments