Breaking News

Makamba kuhusu matumizi ya mkaa, uchumi na mazingira



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba akizungumza katika mdahalo wa Jukwaa la Fikra kujadili matumizi ya mkaa, uchumi na mazingira yetu, jijini Dar es Salaam leo amesema.

“Thamani ya bishara ya mkaa ni kubwa kuliko kahawa lakini pia tembo mkubwa katika mazingira yetu. Kwa upande mwingne Mkaa unaua watu 60 kwa siku lakini pia  Ukivuta Moshi wa mkaa ni sawa na kuvuta pakiti mbili za sigara kwa siku”

“Ukiwauliza watu kwa nini wanatumia mkaa majibu yatakuwa ni;
~ Unapatikana kwa bei rahisi
~Unapatikana kirahisi
~Unapatikana katika vifingashio rahisi”- Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),


"Mkaa sio nafuu kwa sababu bei yake haipimwi kihalali, lakini pia sio nafuu maana unaathiri afya zetu. Tanzania ni mojawapo ya nchi tano Duniani inazoongoza kwa ukataji wa miti na misitu”-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),

"Watu 22,000 wanakufa kila mwaka nchini kutokana na matumizi ya mkaa na kuni. Hiyo ni sawa na watu 60 kwa siku"


“Thamani ya biashara ya mkaa ni kubwa kuliko kahawa na chai kwahiyo mkaa ni sehemu kubwa sana ya uchumi wa nchi yetu kwa namna moja au nyingine, na ni tembo mkubwa katika uchumi wetu".- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),


"Chuo cha #Dodoma kina wanafunzI 27,000. chakula chao kinapikwa kwa kutumia nishati mbadala. Sekta binafsi ina mchango mkubwa katika kutafuta matumizi ya nishati mbadala”- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),

No comments