Yanga yamteua Naibu Waziri Mavunde
Yanga imetangaza leo kamati hiyo ambayo kazi yake maalum ni kusimamia kampeni hiyo ya kuchangisha fedha kwaajili ya kusaidia timu hiyo ambayo inaelezwa kutokuwa vizuri kiuchumi katika misimu ya hivi karibuni.
Naibu Waziri Mavunde, atasaidiwa na makamu mwenyekiti, Lucas Mashauri huku katibu akiwa ni Deo Mutta.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa kamati itakuwa na jumla ya wajumbe 24.
Hivi karibuni Yanga iliwateua wabunge Venance Mwamoto wa Kilolo, Seif Gulamali wa Igunga, Dustan Kitandula wa Mkinga Tanga na Said Mtanda ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Nkasi katika kamati yao ya uchaguzi.
No comments